[104] Na hawa makafiri wakiambiwa: Njooni kwenye yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu katika Qur'ani, na aliyo yaeleza Mtume, ili mpate kuongoka kwa kuyafuata, wao husema: Yanatutosha tuliyo wakuta nayo baba zetu. Yawafalia hawa kusema hayo? Ijapo kuwa hao baba zao ni kama nyama hoa, hawajui lolote la haki, wala hawaijui njia ya kuendea yaliyo sahihi.