Firo maanaaji al-quraan tedduɗo oo - Eggo e ɗemngal Swahili - Ali Muhsin Alberwani.

external-link copy
24 : 3

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ قَالُواْ لَن تَمَسَّنَا ٱلنَّارُ إِلَّآ أَيَّامٗا مَّعۡدُودَٰتٖۖ وَغَرَّهُمۡ فِي دِينِهِم مَّا كَانُواْ يَفۡتَرُونَ

Hayo ni kwa sababu walisema: Hautatugusa Moto isipo kuwa kwa siku chache tu. Na yakawadanganya katika dini yao yale ambayo wenyewe waliyo kuwa wakiyazua. info

Hao wanao kataa miongoni mwa Mayahudi wamedanganyika kwa kukataa kwao na matumaini ya uwongo wanao jitamanisha nafsi zao ya kuwa Moto hautawagusa ila siku chache tu. Na kudanganyika huko na matamanio hayo yamewapelekea kuendelea kuzua katika dini yao kunako endelea.

التفاسير: