Firo maanaaji al-quraan tedduɗo oo - Eggo e ɗemngal Swahili - Ali Muhsin Alberwani.

external-link copy
69 : 12

وَلَمَّا دَخَلُواْ عَلَىٰ يُوسُفَ ءَاوَىٰٓ إِلَيۡهِ أَخَاهُۖ قَالَ إِنِّيٓ أَنَا۠ أَخُوكَ فَلَا تَبۡتَئِسۡ بِمَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Na walipo ingia kwa Yusuf alimchukua nduguye akasema: Mimi hakika ni nduguyo. Basi usihuzunike kwa waliyo kuwa wakiyafanya. info

Walipo ingia kwa Yusuf aliwapokea kwa hishima, na khasa yule nduguye kwa baba na mama ndio akamchukua na akampa siri kwa kumwambia: Usitie shaka mimi ni nduguyo Yusuf. Basi usihuzunike kwa waliyo kufanyia wewe na waliyo nifanyia mimi.

التفاسير: