Firo maanaaji al-quraan tedduɗo oo - Eggo (nantino) ngo e Swahiliire - Abdullah Muhammad e Naasir Khamis.

external-link copy
33 : 6

قَدۡ نَعۡلَمُ إِنَّهُۥ لَيَحۡزُنُكَ ٱلَّذِي يَقُولُونَۖ فَإِنَّهُمۡ لَا يُكَذِّبُونَكَ وَلَٰكِنَّ ٱلظَّٰلِمِينَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ يَجۡحَدُونَ

Hakika sisi tunajua kwamba msimamo wa kaumu zako wa kukukanusha waziwazi unakutia huzuni moyoni mwako. Basi subiri na ujitulize. Kwani wao hawakukanushi wewe kutoka ndani ya roho zao; wao waamini ukweli wako, lakini wao kwa udhalimu na uadui walionao, wanazikataa hoja zilizo wazi zinazoonyesha ukweli wako, ndipo wakakufanya mrongo kwa yale uliyokuja nayo. info
التفاسير: