ترجمهٔ معانی قرآن کریم - ترجمه‌ى سواحلی ـ علی محسن البروانی

Al-Balad

external-link copy
1 : 90

لَآ أُقۡسِمُ بِهَٰذَا ٱلۡبَلَدِ

Naapa kwa Mji huu! info

Naapa kiapo cha mkazo kwa mji wa Makka, mji mtakatifu;

التفاسير:

external-link copy
2 : 90

وَأَنتَ حِلُّۢ بِهَٰذَا ٱلۡبَلَدِ

Nawe unaukaa Mji huu. info

Na wewe unaishi katika mji huu, unauzidisha utukufu wake na cheo chake.

التفاسير:

external-link copy
3 : 90

وَوَالِدٖ وَمَا وَلَدَ

Na naapa kwa mzazi na alicho kizaa. info

Na naapa kwa mzazi na anacho kizaa, na kwa hao wawili ndio jinsi inahifadhika na maendeleo yanabakia.

التفاسير:

external-link copy
4 : 90

لَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ فِي كَبَدٍ

Hakika tumemuumba mtu katika taabu. info

Hakika Sisi tumemuumba mtu katika mashaka na taabu tangu mwanzo wake mpaka kumalizika mambo yake.

التفاسير:

external-link copy
5 : 90

أَيَحۡسَبُ أَن لَّن يَقۡدِرَ عَلَيۡهِ أَحَدٞ

Ati anadhani hapana yeyote ataye muweza? info

Je! Anadhani mtu aliye umbwa katika mashaka haya kuwa hapana awezae kumdhalilisha?

التفاسير:

external-link copy
6 : 90

يَقُولُ أَهۡلَكۡتُ مَالٗا لُّبَدًا

Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali. info

Anasema: Nimetumia katika kupambana na Muhammad s.a.w. na kuupinga wito wake mali mengi ukiyakusanya pamoja.

التفاسير:

external-link copy
7 : 90

أَيَحۡسَبُ أَن لَّمۡ يَرَهُۥٓ أَحَدٌ

Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona? info

Ati anadhani kwamba mambo yake hayo yamefichikana, hayajui yeyote hata huyo aliye muumba?

التفاسير:

external-link copy
8 : 90

أَلَمۡ نَجۡعَل لَّهُۥ عَيۡنَيۡنِ

Kwani hatukumpa macho mawili? info

Kwani Sisi hatukumuumba na macho mawili ya kutazamia,?

التفاسير:

external-link copy
9 : 90

وَلِسَانٗا وَشَفَتَيۡنِ

Na ulimi, na midomo miwili? info

Na ulimi na midomo miwili ili aweze kutamka na kusema sawa?

التفاسير:

external-link copy
10 : 90

وَهَدَيۡنَٰهُ ٱلنَّجۡدَيۡنِ

Na tukambainishia zote njia mbili? info

Na tukamwonyesha njia ya kheri na ya shari, na tukamtengenezea aweze kuchagua mojawapo?

التفاسير:

external-link copy
11 : 90

فَلَا ٱقۡتَحَمَ ٱلۡعَقَبَةَ

Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani. info

Basi huyo hakunafiika kwa tuliyo mtengenezea, wala hakuivuka njia ya milimani inayo mzuia asifikie uwokovu, nayo ni choyo wa nafsi yake.

التفاسير:

external-link copy
12 : 90

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡعَقَبَةُ

Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani? info

Na kitu gani kitakufunza nini huko kujitoma kwenye njia ya milimani?

التفاسير:

external-link copy
13 : 90

فَكُّ رَقَبَةٍ

Kumkomboa mtumwa; info

Kumkomboa mtu kutokana na utumwa,

التفاسير:

external-link copy
14 : 90

أَوۡ إِطۡعَٰمٞ فِي يَوۡمٖ ذِي مَسۡغَبَةٖ

Au kumlisha siku ya njaa info

Au kumlisha siku ya njaa

التفاسير:

external-link copy
15 : 90

يَتِيمٗا ذَا مَقۡرَبَةٍ

Yatima aliye jamaa, info

Yatima aliye jamaa wa kumliwaza kwa ujamaa na ufakiri.

التفاسير:

external-link copy
16 : 90

أَوۡ مِسۡكِينٗا ذَا مَتۡرَبَةٖ

Au masikini aliye vumbini. info

Au masikini mwingi wa haja na kufakirika.

التفاسير:

external-link copy
17 : 90

ثُمَّ كَانَ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَتَوَاصَوۡاْ بِٱلصَّبۡرِ وَتَوَاصَوۡاْ بِٱلۡمَرۡحَمَةِ

Tena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana. info

Tena awe pamoja na hayo miongoni mwa wenye Imani wanao usiana na wenzao kwa subira na kuoneana huruma.

التفاسير:

external-link copy
18 : 90

أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ

Hao ndio watu wa kheri wa kuliani. info

Hao wanao sifika kwa sifa hizi, ndio watu wa kheri, wa mkono wa kulia.

التفاسير:

external-link copy
19 : 90

وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِـَٔايَٰتِنَا هُمۡ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ

Lakini walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni. info

Na walio zikataa dalili tulizo zisimamisha kuthibitisha Haki kutoka na Kitabu na hoja zake, hao ndio wapotovu watu waovu walio kosa kheri na watapata adhabu.

التفاسير:

external-link copy
20 : 90

عَلَيۡهِمۡ نَارٞ مُّؤۡصَدَةُۢ

Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande. info

Juu yao utakuwa Moto ulio bebeana na milango yake ikafungwa.

التفاسير: