ترجمهٔ معانی قرآن کریم - ترجمه‌ى سواحلی ـ علی محسن البروانی

An-Nur

external-link copy
1 : 24

سُورَةٌ أَنزَلۡنَٰهَا وَفَرَضۡنَٰهَا وَأَنزَلۡنَا فِيهَآ ءَايَٰتِۭ بَيِّنَٰتٖ لَّعَلَّكُمۡ تَذَكَّرُونَ

HII NI SURA Tuliyo iteremsha na tukailazimisha; tukateremsha ndani yake Aya zilizo wazi ili mkumbuke. info

Sura hii tumeifunua na tumewajibisha hukumu zake, na tumeteremsha ndani yake dalili zilizo wazi za kuthibitisha uwezo wa Mwenyezi Mungu na upweke wake, na kwamba Kitabu hichi kinatoka kwake, ili mpate kuwaidhika.

التفاسير: