ترجمهٔ معانی قرآن کریم - ترجمه‌ى سواحلى - عبد الله محمد و ناصر خميس

external-link copy
29 : 8

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِن تَتَّقُواْ ٱللَّهَ يَجۡعَل لَّكُمۡ فُرۡقَانٗا وَيُكَفِّرۡ عَنكُمۡ سَيِّـَٔاتِكُمۡ وَيَغۡفِرۡ لَكُمۡۗ وَٱللَّهُ ذُو ٱلۡفَضۡلِ ٱلۡعَظِيمِ

Enyi wale ambao mlimuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakazifuata sheria Zake kivitendo, mkimuogopa Mwenyezi Mungu, kwa kufanya maamrisho Yake na kuepuka makatazo Yake, Atawafanya muwe na upambanuzi baina ya ukweli na urongo, Atawafutia madhambi yenu yaliyopita na Atawafinikia, Hatawaadhibu kwayo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye hisani na vipewa vyingi vyenye kuenea. info
التفاسير: