ترجمهٔ معانی قرآن کریم - ترجمه‌ى سواحلى - عبد الله محمد و ناصر خميس

Ghafir

external-link copy
1 : 40

حمٓ

«Ḥā, Mīm» Yametangulia maelezo kuhusu herufi zilizokatwa na kutengwa mwanzo wa sura ya Al-Baqarah. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 40

تَنزِيلُ ٱلۡكِتَٰبِ مِنَ ٱللَّهِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡعَلِيمِ

Kuteremshiwa Qur’ani Nabii Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kunatokana na Mwenyezi Mungu, Aliyeshinda na kutukuka, Mwenye ushindi Ambaye kwa enzi Yake amekilazimisha kila kiumbe, Mwenye ujuzi wa kila kitu. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 40

غَافِرِ ٱلذَّنۢبِ وَقَابِلِ ٱلتَّوۡبِ شَدِيدِ ٱلۡعِقَابِ ذِي ٱلطَّوۡلِۖ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ إِلَيۡهِ ٱلۡمَصِيرُ

Mwenye kusamehe dhambi za wafanya dhambi, Mwenye kukubali toba ya wenye kutubia, Mkali wa kutesa juu ya aliyejasiri kufanya dhambi na kutotubia kutokana nayo. Na Yeye. Kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Ndiye Mwenye kuwaneemesha na kuwafadhili waja Wake watiifu. Hakuna muabudiwa yoyote anayefaa kuabudiwa isipokuwa Yeye. Kwake Yeye ndio mwisho wa viumbe wote Siku hiyo ya Hesabu, ili Amlipe kila mmoja kile anachostahiki. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 40

مَا يُجَٰدِلُ فِيٓ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ إِلَّا ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فَلَا يَغۡرُرۡكَ تَقَلُّبُهُمۡ فِي ٱلۡبِلَٰدِ

Hakuna anayeteta kuhusu aya za Mwenyezi Mungu na dalili Zake za kutolea ushahidi umoja wa Mwenyezi Mungu, akawa anazikabili kwa ubatilifu isipokuwa wapinzani wenye kukataa kuwa Yeye Ndiye Mola wa kweli Anayestahiki kuabudiwa Peke Yake. Basi kusikudanganye wewe kule kutanga kwao mijini kwa aina mbalimbali za biashara, shughuli za kuchuma, starehe za ulimwenguni na uzuri wake. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 40

كَذَّبَتۡ قَبۡلَهُمۡ قَوۡمُ نُوحٖ وَٱلۡأَحۡزَابُ مِنۢ بَعۡدِهِمۡۖ وَهَمَّتۡ كُلُّ أُمَّةِۭ بِرَسُولِهِمۡ لِيَأۡخُذُوهُۖ وَجَٰدَلُواْ بِٱلۡبَٰطِلِ لِيُدۡحِضُواْ بِهِ ٱلۡحَقَّ فَأَخَذۡتُهُمۡۖ فَكَيۡفَ كَانَ عِقَابِ

Walikanusha, kabla ya makafiri hawa, watu wa Nūḥ na waliowafuata wao miongoni mwa ummah waliotangaza vita vyao dhidi ya Mitume, kama vile 'Ād na Thamūd, kwa kuwa waliazimia kuwaudhi na wakaamua kwa umoja wao wawaadhibu au wawaue. Na kila watu, miongoni mwa ummah hawa wenye kuwakanusha Mitume wao, walitaka kumuua Mtume wao na wakajadiliana na yeye kwa njia ya ubatilifu ili waitangue haki kwa kujadili kwao, na kwa hivyo nikawatesa. Basi ni namna gani kule kuwatesa kwangu kulikuwa ni mazingatio kwa viumbe na mawaidha kwa watakaokuja baada yao? info
التفاسير:

external-link copy
6 : 40

وَكَذَٰلِكَ حَقَّتۡ كَلِمَتُ رَبِّكَ عَلَى ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَنَّهُمۡ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِ

Na kama yalivyothibiti mateso kwa ummah waliopita waliowakanusha Mitume wao, pia yalithibiti kwa wale waliokufuru kuwa wao ni watu wa Motoni. info
التفاسير:

external-link copy
7 : 40

ٱلَّذِينَ يَحۡمِلُونَ ٱلۡعَرۡشَ وَمَنۡ حَوۡلَهُۥ يُسَبِّحُونَ بِحَمۡدِ رَبِّهِمۡ وَيُؤۡمِنُونَ بِهِۦ وَيَسۡتَغۡفِرُونَ لِلَّذِينَ ءَامَنُواْۖ رَبَّنَا وَسِعۡتَ كُلَّ شَيۡءٖ رَّحۡمَةٗ وَعِلۡمٗا فَٱغۡفِرۡ لِلَّذِينَ تَابُواْ وَٱتَّبَعُواْ سَبِيلَكَ وَقِهِمۡ عَذَابَ ٱلۡجَحِيمِ

Wale wanaoibeba ‘Arshi ya Mwenyezi Mungu miongoni mwa Malaika na wale walioko pambizoni mwake kati ya wale wanaoizunguka miongoni mwao, wanamtakasa Mwenyezi Mungu na kila kasoro, wanamshukuru kwa yale Anayostahiki, wanamuamini Yeye haki ya kumuamini na wanamuomba Awasamehe Waumini kwa kusema, «Mola wetu! Umekienea kile kitu kwa rehema na ujuzi. Kwa hivyo wasamehe wale waliotubia kutokana na ushirikina na maasia na wakafuata njia uliyowaamrisha waifuate, nayo ni Uislamu, na uwaepushie adhabu ya Moto na vituko vyake. info
التفاسير: