আল-কোৰআনুল কাৰীমৰ অৰ্থানুবাদ - শ্বাহিলি অনুবাদ- আব্দুল্লাহ মুহাম্মদ আৰু নাচিৰ খামীছ

Az-Zumar

external-link copy
1 : 39

تَنزِيلُ ٱلۡكِتَٰبِ مِنَ ٱللَّهِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَكِيمِ

Kuteremshwa Qur’ani, Hakika ni kwamba, ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu Aliye Mshindi katika uweza Wake na utesaji Wake, Mwingi wa hekima katika uendeshaji mambo Wake na hukumu Zake. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 39

إِنَّآ أَنزَلۡنَآ إِلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ بِٱلۡحَقِّ فَٱعۡبُدِ ٱللَّهَ مُخۡلِصٗا لَّهُ ٱلدِّينَ

Kwa hakika sisi tumekuteremshia, ewe Mtume, Qur’ani inayoamuru haki na uadilifu. Basi muabudu Mwenyezi Mungu, Peke Yake, na umtakasie mambo yote ya Dini yako. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 39

أَلَا لِلَّهِ ٱلدِّينُ ٱلۡخَالِصُۚ وَٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُواْ مِن دُونِهِۦٓ أَوۡلِيَآءَ مَا نَعۡبُدُهُمۡ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَآ إِلَى ٱللَّهِ زُلۡفَىٰٓ إِنَّ ٱللَّهَ يَحۡكُمُ بَيۡنَهُمۡ فِي مَا هُمۡ فِيهِ يَخۡتَلِفُونَۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي مَنۡ هُوَ كَٰذِبٞ كَفَّارٞ

Jua utanabahi kwamba ni haki ya Mwenyezi Mungu, Peke Yake, kutiiwa utiifu uliyotimia uliosalimika na ushirikina. Na wale wanaomshirikisha mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu wakawafanya wasiokuwa Yeye kuwa ni wategemewa, wanasema, «Hatuwaabudu waungu hawa pamoja na Mwenyezi Mungu isipokuwa wapate kutuombea kwa Mwenyezi Mungu na ili watukurubishe daraja Kwake.» Hivyo basi wakakufuru, kwani ibada na uombezi ni wa Mwenyezi Mungu, Peke Yake. Hakika Mwenyezi Mungu Atawapambanua, Siku ya Kiyama, baina ya Waumini wenye ikhlasi na wale wenye kumshirikisha mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu, katika yale waliokuwa wanatafautiana juu yake kuhusu vile walivyoabudu. Hapo amlipe kila mmoja kwa anachostahiki. Hakika Mwenyezi Mungu hawaelekezi kuongoka kwenye njia iliyonyoka wale wenye kumzulia urongo Mwenyezi Mungu, wenye kuzikanusha aya Zake na hoja Zake. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 39

لَّوۡ أَرَادَ ٱللَّهُ أَن يَتَّخِذَ وَلَدٗا لَّٱصۡطَفَىٰ مِمَّا يَخۡلُقُ مَا يَشَآءُۚ سُبۡحَٰنَهُۥۖ هُوَ ٱللَّهُ ٱلۡوَٰحِدُ ٱلۡقَهَّارُ

Lau Angalitaka Mwenyezi Mungu kuwa na mtoto, Angalichagua, miongoni mwa viumbe Vyake, Anachotaka. Ameepukana Mwenyezi Mungu na kutakasika na kuwa na mtoto! Hakika Yeye ni Mmoja Aliye Pekee na kupwekeka, Mwenye kutegemewa kwa kila haja, Mwenye kutendesha nguvu ambaye Amewalazimisha viumbe kwa uweza Wake, basi kila kitu kinamdhalilikia Yeye na kumnyenyekea. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 39

خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ بِٱلۡحَقِّۖ يُكَوِّرُ ٱلَّيۡلَ عَلَى ٱلنَّهَارِ وَيُكَوِّرُ ٱلنَّهَارَ عَلَى ٱلَّيۡلِۖ وَسَخَّرَ ٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَۖ كُلّٞ يَجۡرِي لِأَجَلٖ مُّسَمًّىۗ أَلَا هُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡغَفَّٰرُ

Ameumba Mwenyezi Mungu mbingu na ardhi na viliyomo ndani yake, Anauleta usiku na kuuondoa mchana, na Anauleta mchana na kuuondoa usiku. Na Amelidhalilisha jua na mwezi ili manufaa ya waja yapangike. Kila mojawapo ya hivi viwili vinatembea kwenye sehemu yake ya kuzunguka mpaka kipindi cha kusimama Kiyama. Jua utanabahi, hakika Mwenyezi Mungu Aliyefanya matendo haya na Akawapa waja Wake neema hizi, Ndiye Mshindi juu ya viumbe Vyake, ni Mwingi wa kusamehe dhambi zao. info
التفاسير: