ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាswahili - អាប់ឌុលឡោះ ម៉ូហាំម៉ាត់ និងណាសៀរ ខមុីស

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
24 : 29

فَمَا كَانَ جَوَابَ قَوۡمِهِۦٓ إِلَّآ أَن قَالُواْ ٱقۡتُلُوهُ أَوۡ حَرِّقُوهُ فَأَنجَىٰهُ ٱللَّهُ مِنَ ٱلنَّارِۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ

Basi jawabu ya watu wa Ibrāhīm haikuwa isipokuwa ni kuambiana wao kwa wao, «Muueni au mchomeni kwa moto!» Wakamtupa motoni, na Mwenyezi Mungu Akamuokoa nao, na akaufanya kuwa ni baridi na salama kwake. Hakika katika kumuokoa kwetu Ibrāhīm kutokana na moto pana dalili na hoja kwa watu wanaomuamini Mwenyezi Mungu na kufanya matendo yanayoambatana na Sheria Yake. info
التفاسير:

external-link copy
25 : 29

وَقَالَ إِنَّمَا ٱتَّخَذۡتُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ أَوۡثَٰنٗا مَّوَدَّةَ بَيۡنِكُمۡ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۖ ثُمَّ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ يَكۡفُرُ بَعۡضُكُم بِبَعۡضٖ وَيَلۡعَنُ بَعۡضُكُم بَعۡضٗا وَمَأۡوَىٰكُمُ ٱلنَّارُ وَمَا لَكُم مِّن نَّٰصِرِينَ

Na Akasema Ibrāhīm kuwaambia watu wake, «Enyi watu wangu! Kwa hakika, nyinyi mumewaabudu waungu wa ubatilifu, mumewafanya wao ni waabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu, mnapendana juu ya kuwaabudu na mnajipendekeza kwa kuwatumikia. Kisha, Siku ya Kiyama, baadhi yenu watajiepusha na wengine na mtalaaniana nyinyi kwa nyinyi, na mwisho wenu ni Moto, na hamtakuwa na msaidizi wa kuwazuia kuuingia. info
التفاسير:

external-link copy
26 : 29

۞ فَـَٔامَنَ لَهُۥ لُوطٞۘ وَقَالَ إِنِّي مُهَاجِرٌ إِلَىٰ رَبِّيٓۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Lūṭ akamuamini Ibrāhīm na akaufuata mwenendo wake. Na Ibrāhīm akasema, «Mimi nitaiwacha nchi ya watu wangu na nitaenda kwenye ardhi iliyobarikiwa, nayo ni Shām, kwani Mwenyezi Mungu ni Mshindi Asiyeshindwa ni Mwingi wa hekima katika uendeshaji mambo Wake. info
التفاسير:

external-link copy
27 : 29

وَوَهَبۡنَا لَهُۥٓ إِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَ وَجَعَلۡنَا فِي ذُرِّيَّتِهِ ٱلنُّبُوَّةَ وَٱلۡكِتَٰبَ وَءَاتَيۡنَٰهُ أَجۡرَهُۥ فِي ٱلدُّنۡيَاۖ وَإِنَّهُۥ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ لَمِنَ ٱلصَّٰلِحِينَ

Na tukamtunukia yeye Isḥāq, mtoto wake, na Y'qub, mtoto wa mtoto wake. Na tukawafanya, katika kizazi chake, Mitume na tukawaletea Vitabu. Na tukampa yeye malipo mema ya mitihani aliyoipata kwa ajili yetu, nayo ni kutajwa vizuri na kuwa na wana wema duniani. Na kwa hakika, yeye huko Akhera ni miongoni mwa watu wema. info
التفاسير:

external-link copy
28 : 29

وَلُوطًا إِذۡ قَالَ لِقَوۡمِهِۦٓ إِنَّكُمۡ لَتَأۡتُونَ ٱلۡفَٰحِشَةَ مَا سَبَقَكُم بِهَا مِنۡ أَحَدٖ مِّنَ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Mkumbuke na umtaje Lūṭ, ewe Mtume, alipowaambia watu wake, «Kwa hakika, nyinyi mnaleta kitendo kichafu, hakuna yoyote katika viumbe aliyetangulia kukifanya. info
التفاسير:

external-link copy
29 : 29

أَئِنَّكُمۡ لَتَأۡتُونَ ٱلرِّجَالَ وَتَقۡطَعُونَ ٱلسَّبِيلَ وَتَأۡتُونَ فِي نَادِيكُمُ ٱلۡمُنكَرَۖ فَمَا كَانَ جَوَابَ قَوۡمِهِۦٓ إِلَّآ أَن قَالُواْ ٱئۡتِنَا بِعَذَابِ ٱللَّهِ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ

Je, ni vipi nyinyi mnawajilia wanaume kupitia sehemu zao za nyuma, mnavamia njia za wasafiri kwa kitendo chenu kiovu na mnafanya vitendo vibaya kwenye mabaraza yenu, kama vile kuwacheza shere watu, kuwarushia mawe wapita njia na kuwakera kwa maneno na vitendo kwa namna isiyofaa?» Katika haya kuna tangazo kwamba haifai watu kukusanyika juu ya jambo baya ambalo Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wamelikataza. Watu wa Lūṭ hawakuwa na jawabu la kumpa isipokuwa ni kusema, «tuletee adhabu ya Mwenyezi Mungu ikiwa wewe ni miongoni mwa wakweli katika hayo unayoyasema na ni miongoni mwa watekelezaji katika ahadi unayoitoa.» info
التفاسير:

external-link copy
30 : 29

قَالَ رَبِّ ٱنصُرۡنِي عَلَى ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡمُفۡسِدِينَ

Akasema, «Mola wangu! Nipe ushindi juu ya watu waharibifu kwa kuwateremshia adhabu, kwa kuwa wameuzua uchafu huu na wameendelea nao» Na Mwenyezi Mungu Akaikubali dua yake. info
التفاسير: