Traduction des sens du Noble Coran - La traduction swahilie - 'Alî Muhsin Al Barwânî

external-link copy
5 : 21

بَلۡ قَالُوٓاْ أَضۡغَٰثُ أَحۡلَٰمِۭ بَلِ ٱفۡتَرَىٰهُ بَلۡ هُوَ شَاعِرٞ فَلۡيَأۡتِنَا بِـَٔايَةٖ كَمَآ أُرۡسِلَ ٱلۡأَوَّلُونَ

Lakini wao walisema: Hizo ni ndoto za ovyo ovyo, bali amezizua tu, bali huyo ni mtunga mashairi. Basi atuletee miujiza kama walivyo tumwa wale wa mwanzo. [5] info

[5] Bali wao wakasema: Hizi ni mchanganyiko wa ndoto alizo ziota (Muhammad); bali kazua tu na akamsingizia Mwenyezi Mungu kwa uwongo. Kisha wakaacha hayo na wakasema: Bali huyu ni mtunga mashairi anaziteka nafsi za wenye kumsikiliza. Kama kweli, basi na atuletee muujiza khasa wa kuonyesha ukweli wake, kama walivyo tumwa Manabii wa zamani wakitiwa nguvu kwa miujiza mbali mbali.

التفاسير: